14 C
New York

Mahrez atangaza kustaafu soka mwakani

Published:

ALGIERS, Algeria
MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Algeria, Riyad Mahrez, ameweka wazi kuwa fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakuwa za mwisho katika maisha yake ya soka.
Kwa mujibu wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, atatundika daluga baada ya michuano hiyo itakayofanyika katika nchi tatu (Marekani, Mexico na Canada).
Mahrez anayeitumikia klabu ya Al-Ahli ya Saudi Arabia, ametangaza hivyo baada ya kuiongoza Algeria kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo kwa mara ya tano.
Staa huyo alifunga bao moja na kutoa ‘asisti’ mbili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Somalia na matokeo hayo yakaiwezesha Algeria kukata tiketi ikiwa kileleni mwa Kundi G.
“Hizi zitakuwa fainali zangu za mwisho za Kombe la Dunia,” amesema Mahrez na kuongeza kuwa yeye si Cristiano Ronaldo anayeendelea kucheza soka akiwa na umri wa miaka 40.
Akiwa anatarajia kutimiza umri wa miaka 35 ifikapo Februari, mwakani, Mahrez ameshafunga mabao 33 katika mechi 106 alizocheza tangu alipoanza kuitumikia Algeria.
Algeria, licha ya kushiriki mara nne (1982, 1986, 2010 na 2014), mafanikio makubwa zaidi kwao kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia ni kufika hatua ya 16 bora mwaka 2014.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img