RIYADH, Saudi Arabia
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ameandika historia ya kuwa bilionea wa kwanza kwa upande wa wachezaji mpira wa miguu.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya taasisi maarufu ya masuala ya fedha ya Bloomberg.
Ronaldo amefikia hapo kutokana na mishahara, posho na mapato anayovuna katika dili za matangazo na uwekezaji.
Kwa makusanyo ya vyanzo hivyo vya mapato, Ronaldo anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia ana utajiri wa Pauni bilioni 1.04.
Kwa mujibu wa Bloomberg, nyota huyo mwenye umri wa miaka 40, alivuna mshahara wa Pauni milioni 410 kati ya mwaka 2002 na 2023.
Wakati huo huo, nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno anachota Pauni milioni 13.4 kutokana na mkataba wake na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike.
Published:


