10.9 C
New York

Bayern yaivamia Liver kwa Guehi

Published:

MUNICH, Ujerumani

VIGOGO wa Bundesliga, Bayern Munich, wamejitosa katika mpango wa Liverpool wa kumsajili beki wa Crystal Palace, Marc Guehi.
Guehi mwenye umri wa miaka 25, ni nahodha wa Palace na alikiongoza kikosi hicho kunyakua ubingwa wa Kombe la FA msimu uliopita.
Taarifa zinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern, Max Eberl, ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo na amepanga kuinasa saini yake ifikapo Januari, mwakani.
Mkataba wake wa sasa na Palace utafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu na Liverpool walijaribu bila mafanikio kumnasa wakati wa usajili wa majira haya ya kiangazi.
Saa chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa, kocha wa Palace, Oliver Glasner, alizuia dili hilo kufanyika.
Glasner alikataa biashara kufanyika kwa kuwa mabosi wa Palace hawakuwa wamesajili beki wa kati wa kuchukua nafasi ya Guehi.
Wakati huo huo, Liverpool wanaripotiwa kutokukata tamaa katika mpango wa kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa England.
Katika hatua nyingine, vigogo wengine wa soka la Ulaya, Real Madrid, nao wametajwa kuipigia hesabu huduma ya Guehi, ingawa bado Liverpool inapewa nafasi kubwa zaidi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img