10.9 C
New York

Mbwa amponza staa West Ham United

Published:

LONDON, Uingereza
NYOTA wa zamani wa West Ham United ya England, Said Benrahma, amefunguliwa mashitaka baada ya mbwa wake kumng’ata mtembea kwa miguu.
Benrahma (30), ambaye alicheza West Ham kwa misimu minne, kwa sasa anakipiga Ligi Kuu ya Saudi Arabia.
Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo ameshitakiwa kwa kosa la uzembe uliosababisha mbwa huyo kusababisha madhara.
Hata hivyo, kosa hilo lilitokea mwaka 2023, wakati huo Benrahma akiishi Hornchurch, London.
Endapo atakutwa na hatia, huenda akafungwa jela, akatozwa faini au kupigwa marufuku kumiliki mbwa.
Wakati wa usikilizaji wa kesi yake, Benrahma hakuwepo mahakamani na aliyemshitaki ni mwanaume aliyefahamika kwa jina la Luke Rehbin.
Baadaye mwezi huu, Benrahma ataazimika kufika mahakamani au kutumia njia ya video kusikiliza kesi yake ikisomwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img