11.7 C
New York

Timu 64 kushiriki Kombe la Dunia

Published:

NYON, Uswis
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) linatazamia kufikisha timu 64 zitakazokuwa zikishiriki fainali za Kombe la Dunia.
Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya soka, michuano hiyo itakuwa na timu 48 hapo mwakani.
Mpango huo ni matokeo ya viongozi wa FIFA kukutana na marais wa Uruguay na Paraguay mjini New York, mkutano uliowahuhisha pia viongozi wa Shirikisho la Soka Kusini mwa Afrika (CONMEBOL) na Rais wa Chama cha Soka cha Argentina.
Kwa mujibu wa taarifa, FIFA inataka kuona fainali za mwaka 2030, ambapo Shirikisho hilo litakuwa limetimiza miaka 100, zinakuwa na ushiriki wa timu 64.
Akizungumzia hilo, Rais wa CONMEBOL, Alejandro Dominguez, amesema kwa maana halisi ya Kombe la Dunia ni kuona michuano hiyo inakuwa na ushiriki wa timu nyingi kutokana maeneo mengi.
Hata hivyo, wakosoaji wanaona ushiriki wa timu 64 ukisababisha idadi ya mechi kufikia 128, hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa wachezaji.
Mara ya kwanza kuona Kombe la Dunia likiwa na timu 48 ni mwakani, ambapo mechi za michuano hiyo zitachezwa katika mataifa matatu (Marekani, Mexico na Canada).
Ikumbukwe, mara ya mwisho kwa Marekani kuwa mwenyeji wa fainali hizo ilikuwa mwaka 1994, wakati huo idadi ya timu zinazoshiriki ikiwa ni 24.
Kuanzia mwaka 1998, michuano hiyo ilianza kushirikisha timu 32, utaratibu ambao umekuwapo hadi sasa, ikiwamo wakati wa fainali zilizopita za mwaka 2022 nchini Qatar.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img