MONROVIA, Liberia
RAIS wa zamani wa Liberia, George Weah, amekumbana na ukosolewaji mkali kutoka kwa mashabiki baada ya kauli yake ya hivi karibuni.
Weah aliyewahi kucheza AC Milan na kuwa Mwafrika pekee kutwaa Ballon d’Or, amewakera mashabiki wengi baada ya kusema yeye si shabiki wa mchezo huo.
Aliyasema hayo akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Roberts alipokuwa akirejea Liberia akitokea Ufaransa alikokwenda kukamilisha dili la mtoto wake, Timothy Weah, kutua Marseille.
“Licha ya kwamba niliwahi kucheza, mimi si shabiki wa mchezo huo,” alisema Weah akiwaambia waandishi wa Habari.
Mashabiki wamemkejeli mkongwe huyo kwa kumkumbusha kauli aliyoitoa mwaka jana jijini Paris.
Akiwa kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za Ballon d’Or, Weah aliyeibeba mwaka 1995 alijitaja kuwa ni shabiki wa Tottenham tangu akiwa mdogo.
Pia, mashabiki walienda mbali zaidi na kumkumbusha kauli yake ya mwaka 2017, alipojitaja kuwa ni shabiki wa miaka mingi wa vigogo wa soka la Italia, Juventus.
Published:


