11.7 C
New York

Maignan aingia rada za Man United

Published:

TURIN, Italia
KLABU ya Manchester United imeanza kumfuatilia mlinda mlango wa AC Milan, Mike Maignan, licha ya kwamba wana upinzani mkali kutoka kwa Chelsea.
Man United walifunga usajili wa kiangazi kwa kumsajili kipa wa Royal Antwerp, Senne Lammens, lakini kuondoka kwa Andre Onana kunawalazimisha kurudi sokoni Januari, mwakani.
Baada ya kusajiliwa kwa ada kubwa akitokea Inter Milan, akipewa nafasi ya kuchukua nafasi ya David de Gea, Onana alijikuta akishindwa kuonesha kiwango bora alichokuwa nacho Serie A.
Ni kutokana na makosa mengi langoni, Man United ilimfungulia mlango wa kutua Trabzonspor, ingawa ni kwa mkataba wa mkopo mwa msimu mmoja (2025-26).
Katika mechi za hivi karibuni, kocha Ruben Amorim ameonekana kumuamini zaidi Altay Bayindir, ingawa bado haoni kama mlinda mlango huyo raia wa Uturuki anatosha kwa asilimia 100.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img