11.7 C
New York

Locatelli asakwa kila kona England

Published:

TURIN, Italia
SAINI ya kiungo wa Juventus, Manuel Locatelli, inawindwa vikali na klabu za Ligi Kuu ya England, zikiwamo Aston Villa na West Ham United.
Wakati huo huo, mabosi wa Wolves nao wameripotiwa na vyombo vya Habari vya Italia kuwa wameanza kumfuatilia nyota huyo kuelekea usajili wa Januari, mwakani.
Mchezaji huyo raia wa Italia alijiunga na Juventus kwa mkopo mwaka 2021 akitokea Sassuolo, kabla ya klabu hiyo ya Turin kumsajili moja kwa moja miaka miwili baadaye.
Katika mechi zaidi ya 200 alizocheza akiwa na ‘uzi’ wa Juventus, Locatelli ameingia kambani mara sita na kutoa pasi za mabao (asisti) 15.
Juventus wako tayari kukaa mezani na kusikiliza ofa ya klabu yoyote inayomtaka, ikielezwa pia Locatelli naye anavutiwa na mpango wa kuhamia England.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img