11.7 C
New York

Flick afunguka Yamal kukosa Ballon d’Or

Published:

CATALUNYA, Hispania
KOCHA wa Barcelona, Hansi Flick, amesema staa wake, Lamine Yamal, atakuwa bora zaidi kutokana na hasira za kuikosa Ballon d’Or ya mwaka huu.
Yamal mwenye umri wa miaka 18, alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuibeba, ingawa ilitua kwa nyota wa PSG, Ousmane Dembele, ambaye alikuwa moto zaidi msimu uliopita.
Licha ya kuikosa tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Mwaka, Yamal aliyeibuliwa na ‘academy’ ya Barcelona, hakuambulia patupu, na badala yake alitangazwa kuwa Kinda Bora.
Winga huyo aliiongoza Barcelona kumaliza msimu uliopita ikiwa na mataji mawili ya ndani (La Liga, Copa del Rey na Spanish Super Cup).
“Nilizungumza naye na naamini haijamuumiza, nafikiri itamuongezea hasira ya mafanikio zaidi katika miaka ijayo,” alisema Flick kuwaambia waandishi wa habari.
Kwa upande mwingine, Flick raia wa Ujerumani alikiri kuwa Dembele alistahili kuwa mshindi wa mwaka huu wa Ballon d’Or.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img