11.7 C
New York

Burna Boy awakataa Ronaldo, Messi

Published:

LAGOS, Nigeria
SUPASTAA wa muziki wa Afrobeats, Burna Boy, ‘amewapotezea’ Cristiano Ronaldo na Lionel Messi na kumtaja Jay Jay Okocha kuwa ndiye mwanasoka bora wa muda wote.
Burna Boy anafahamika kwa mapenzi yake kwenye soka na tayari anamiliki kituo cha kuibua na kukuza vipaji vya mchezo huo mjini Lagos.
Katika nafasi ya pili, Burna Boy alimtaja Ronaldinho na kuhitimisha na mpachikaji mabao wa timu ya taifa ya Nigeria, Victor Osimhen.
Orodha ya msanii huyo imeibua mjadala mkubwa huko mitandaoni, ikifahamika kuwa Ronaldo na Messi, ambao kwa pamoja wametwaa mara 13 tuzo ya Ballon d’Or kwa miaka 20 ya hivi karibuni.
Ukiacha Okocha na Ronaldinho ambao wameshastaafu, Osimhen mwenye umri wa miaka 26 ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Nigeria.
Kwa upande mwingine, Osimhen anayekipiga Galatasaray, anashikilia tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika na aliingia kwenye kinyang’anyiro cha Ballon d’Or mwaka 2023.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img