ACCRA, Ghana
BONDIA mwenye umri wa miaka 27, Ernest Akushey, ameripotiwa kupoteza maisha, zikiwa ni siku chache tu tangu alipopoteza pambano.
Akushey alidundwa na Jacob Dickson kwa ‘KO’ ya raundi ya nane mjini Accra, pambano lililopigwa Septemba 12. Taarifa zinaeleza kuwa alianza kusikia mwili ukiwa hauko sawa siku 10 baadaye, kabla ya kufariki Jumanne ya wiki hii.
Historia yake katika mchezo huo inaonesha kuwa Akushey alianza kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2019.
Tangu kipindi hicho, hakuwahi kupoteza pambano hadi pale alipotandikwa na Jonathan Tetteh katika ‘vita’ yao ya Mei, mwaka huu.
Miongoni mwa walioeleza kusikitishwa na kifo chake ni mpinzani wake wa pambano la Septemba 12, Dickson, ambaye ametumia mitandao ya kijamii kuandika: “Licha ya kwamba tulikuwa wapinzani ulingoni, nilifahamu kuwa wewe ni bondia bora. Ni Habari mbaya kuona haupo tena.”
Published:


