SEVILLE, Hispania
BAO la dakika ya 85 la winga wa zamani wa Manchester United, Antony, limeiwezesha Real Betis kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Nottingham.
Ni katika mchezo wa jana wa Ligi ya Europa, ambapo wenyeji Betis walitangulia wa bao la mshambuliaji raia wa DRC, Cedric Bakambu, aliyefunga katika dakika ya 15.
Dakika nne tu baadaye, Forest walisazawisha kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Brazil, Igor Jesus.
Katika dakika ya 23, Jesus aliyesajiliwa kwa Pauni milioni 10 akitokea Botafogo, alirudi tena kwenye nyavu za Betis, kabla ya Anthony kuisawazishia timu hiyo ya Hispania.
Ni kwa maana hiyo sasa, kocha mpya wa Forest, Ange Postecoglou, amefikisha mechi nne bila kuonja ushindi tangu aajiriwe kuchukua mikoba ya Nuno Espirito Santo.
Published:


