PARIS, Ufaransa
LUCA Zidane ambaye ni mtoto wa mkongwe Zinedine, amechagua kuitosa Ufaransa na sasa ataonekana akiwa na timu ya taifa ya Algeria.
Nyota huyo anakidhi vigezo hivyo kwa kuwa wazazi wa baba yake, ‘Zizou’, walitokea Algeria.
Luca anayecheza eneo la kipa, ana umri wa miaka 27 na aliwahi kuiwakilisha Ufaransa katika ngazi ya timu za vijana.
Hivyo basi, baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kubariki, huenda Lucas akashiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia akiwa kwenye lango la Algeria.
Kwa sasa, Lucas ambaye ni mmoja ya watoto wanne wa Zidane, ni kipa wa Granada inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Hispania.
Akitokea katika ‘academy’ ya Madrid, aliwahi kukipiga La Liga akiwa na kikosi cha Rayo Vallecano.
Kwa upande wake, Zizou aliamua kuiwakilisha Ufaransa, akipata nafasi ya kucheza mara mbili fainali za Kombe la Dunia.
Hata hivyo, walikosa ubingwa katika michuano hiyo ya mwaka 1998 baada ya kufungwa na Italia katika mchezo wa fainali.
Published:


