PRETORIA, Afrika Kusini
SAA 72 tu baada ya kumfuta kazi Nasreddine Nabi, mabosi wa Kaizer Chiefs wamemtangaza kocha mpya.
Pedro Goncalves, raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 48, ndiye aliyeajiriwa kuchukua mikoba ya kocha huyo wa zamani wa Yanga.
Goncalves ni miongoni mwa makocha wenye ‘CV’ kubwa barani Afrika, akikumbukwa kwa mafanikio yake ya kuifikisha Angola katika hatua ya robo fainali ya AFCON mwaka 2023.
Kama hiyo haitoshi, aliiongoza Angola kutwaa ubingwa wa COSAFA kwa kuifunga Afrika Kusini mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.
Inaelezwa kuwa kabla ya kumalizana na Kaizer, kocha huyo alikuwa kwenye rada za matajiri wa klabu ya Al Ahly.
Published:


