13.4 C
New York

Liverpool na rekodi ya ‘mabao ya jioni’

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza
USHINDI wa bao 1-0 dhidi ya Burnley umeifanya Liverpool kuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu ya England (EPL) kushinda mechi nne mfululizo za mwanzoni mwa msimu.
Katika mchezo huo, Liverpool ilishaelekea kugawana pointi na wapinzani wao hao, kabla ya Mohamed Salah kutikisa nyavu za Burnley katika dakika ya 95.
Kwa upande mwingine, wafuatiliaji wa EPL watagundua kuwa mechi za hivi karibuni zimeshuhudia Liverpool ikipata mabao yake katika ‘dakika za jioni’.
Ndiyo, katika mechi zake dhidi ya Bournemouth na Arsenal, vijana hao wa kocha Arne Slot wakipata mabao baada ya dakika 80.
Kuziweka sawa rekodi, hata katika mechi nyingine ngumu dhidi ya Newcastle United, mabingwa watetezi hao walipata bao la ushindi katika dakika ya 10 kabla ya zile za nyyongeza kumalizika.
Mwendo wao huo si tu kwa msimu huu. Tangu msimu wa 2022-23, Liverpool imefunga mabao 34 baada ya dakika 80. Hakuna timu iliyofikia rekodi hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img