13.4 C
New York

Amorim ajibu mapigo, awavaa wanamkosoa

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema hafikirii kubadili mbinu anazotumia, licha ya wengi kukosoa kiwango cha timu hiyo.
Man United imekuwa na mwanzo mbaya wa msimu huu wa Ligi Kuu ya England, ambapo imeshinda mechi moja tu kati ya nne ilizoshuka dimbani.
Kwa maoni ya wengi, wakiwamo wachambuzi wa mechi za Ligi Kuu hiyo, Amorim anapaswa kuachana na mfumo wake wa 3-4-2-1.
Sasa, wakati wengi wakiponda mbinu zake, raia huyo wa Ureno amesema hatobadilika, hata kama atashauriwa na Papa wa Wakatoliki.
“Hapana, siwezi kubadilisha, hata kama nitashauriwa na Papa…” alisema Amorim, kocha wa zamani wa Sporting Lisbon ya Ureno.
“Hii ni kazi yangu. Ni majukumu yangu. Kwa ufupi, haya ndiyo maisha yangu, hivyo sitaweza kubadilisha chochote.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img