13.4 C
New York

Staa Arsenal akana mashitaka ya ubakaji

Published:

LONDON, Uingereza
KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey, amekanusha mashitaka ya ubakaji yaliyofunguliwa dhidi yake na wanawake wawili.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ghana anatajwa kuhusika katika udhalilishaji huo kuanzia mwaka 2021 hadi 2022.
Kwa mujibu wa taarifa, Partey mwenye umri wa miaka 32 alifanya hayo wakati akiwa mchezaji wa Arsenal.
Itakumbukwa kuwa kesi zilianza siku nne tu baada ya kumaliza mkataba wake na Arsenal na kutua Villareal akiwa mchezaji huru.
Kwa sasa, Partey ameachiwa kwa dhamana hadi kesi yake itakaposikilizwa tena Novemba 2, mwakani.
Hata hivyo, kesi inayoendelea haimzuii kucheza soka, ingawa ni kwa shari la kuitaarifu polisi saa 24 kabla ya safari yoyote ya nje ya Hispania.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img