15.8 C
New York

Yanga yafikisha mabao matano ya ‘derby’

Published:

Na Hassan Mwasha
KATIKA mechi sita za ‘derby’ ya Ngao ya Jamii, imekuwa ni mara ya tatu kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Simba.
Takwimu hizo ni baada ya matokeo ya mchezo wa jana, ambapo Yanga ikiwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ilishinda bao 1-0 kupitia kwa kiungo wake raia wa Ivory Coast, Pacome Zouazoua.
Wakati huo huo, katika mechi sita hizo, Yanga, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wanaongoza kwa mabao ya kufunga, pia wakiwa na wastani mzuri wa kuruhusu nyavu zao kutikiswa.
Takwimu za derby ya Ngao ya Jamii zinaonesha kuwa Yanga imefikisha mabao ya kufunga matano na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara moja tu.
Ngao ya Jamii ni ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Bara unaotarajiwa kuanza Septemba 17, mwaka huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img