15.8 C
New York

Mata wa Chelsea atua kwa wapinzani Australia

Published:

MELBOURNE, Australia
KIUNGO wa zamani wa Chelsea na Manchester United, Juan Mata, amesajiliwa na Melbourne Victory inayoshiriki Ligi Kuu ya Australia.
Msimu uliopita. Mata mwenye umri wa miaka 37 aliwatumikia wapinzani wao, Western Sydney Wanderers.
Hata hivyo, kwa msimu uliopita, aliingia kikosi cha kwanza katika mechi saba pekee.
Akihojiwa baada ya kujiunga na Wanderers, Mata alisema amechukua hatua hiyo ili kupata timu itakayompa nafasi ya kucheza.
“Naamini nitaisaidia timu kupata mataji, pia nikiamini nitakuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu ya klabu.”
Mata alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2010, pia akishinda ubingwa wa Euro mwaka 2012.
Baada ya kung’ara akiwa Valencia, Chelsea ilimsajili mwaka 2011, ambapo aliipa mataji ya Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa na FA.
Akiwa Manchester United iliyomsajili mwaka 2014, alibeba FA, Kombe la Ligi na Ligi ya Europa msimu wa 2016-17.
Alitimka Old Trafford na kupita katika klabu za Galatasaray na Vissel Kobe ya Japan, kabla ya kuhamia Australia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img