15.8 C
New York

Rooney asema Amorim ameshindwa kazi United

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KWA mujibu wa Wayne Rooney, Manchester United imekuwa mbovu zaidi chini ya kocha raia wa Ureno, Ruben Amorim.
Man United, mabingwa mara 20 wa taji la Ligi Kuu ya England, ilimuajiri Amorim mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumfuta Erik ten Hag.
Ikiwa ni miezi zaidi ya 10 sasa tangu alipokalia kiti, Amorim ameonekana kushindwa kuonesha tofauti yake na mtangulizi wake huyo.
Machungu kwa mashabiki yaliongezeka wikiendi iliyopita, baada ya kuishuhudia timu yao ikitandikwa mabao 3-0 na Manchester City.
Wakiwa ugenini katika Uwanja wa Etihad, sehemu kubwa ya mashabiki wa Man United walionekana wakiondoka majukwaani hata kabla ya mchezo kumalizika.
Akizungumzia mwenendo wa timu yake ya zamani, Rooney alisema: “Ukweli ni kwamba ni ngumu kukaa hapa na kusema kuna mabadiliko au kuna dalili za kupata matokeo mazuri hapo baadaye.”
Man United ilimaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya 15 katika msimamo baada ya kukusanya pointi 42 pekee.
Wakati huo huo, klabu hiyo imetumia Pauni milioni 250 katika usajili wa wachezaji tangu Amorim alipoajiriwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img