ATHENS, Ugiriki
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Anthony Martial, amekamilisha usajili wa kujiunga na Monterrey ya Mexico.
Nyota huyo anaungana beki wa zamani wa Real Madrid, Sergio Ramos, ambaye alitua Monterrey ya Mexico mwanzoni mwa mwaka huu.
Martial (29), ambaye alicheza mechi 317 akiwa na Man United ametua Mexico akitokea AEK Athens ya Ugiriki.
Kwa miaka tisa aliyokuwa Man United, straika huyo raia wa Ufaransa alifunga mabao 90.
Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na vyombo vya habari, Martial amesaini mkataba wa miaka miwili na Monterrey.
Baada ya kuondoka Old Trafford akiwa mchezaji huru mwaka 2024, alifunga mabao saba katika mechi 19 za Ligi Kuu ya Ugiriki.
Itakumbukwa, Martial aliweka rekodi ya kuwa kinda wa bei mbaya zaidi duniani aliposajiliwa na Man United kwa Pauni milioni 36 akitokea Monaco mwaka 2015.
Published:


