15.8 C
New York

Ngao ya Jamii Zanzibar kuchezwa kesho

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
MCHEZO wa Ngao ya Jamii kati ya Mlandege FC na KMKM SC unatarajiwa kuchezwa kesho katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mtanange huo ni ufunguzi wa msimu mpya wa 2025-26 wa Ligi Kuu Visiwani humo.
Ifahamike kuwa mechi za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu zitaanza kuchezwa Septemba 20, mwaka huu.
Katika taarifa yake ya leo Septemba 13, Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) limewaomba mashabiki kuhudhuria kwa wingi uwanjani ili kushuhudia mechi hiyo.
Aidha, ZFF imetangaza viingilio kuwa ni Shilingi 1,000 kwa majukwaa ya Urusi, Saa na Orbit.
Kwa upande mwingine, Shirikisho limeweka wazi kuwa kiingilio kwa Jukwaa la Wings ni Shilingi 30,000.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img