15.8 C
New York

Mtaalamu wa usajili Arsenal kutua Brighton

Published:

LONDON, Uingereza
ALIYEWAHI kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal, Jason Ayto, anajiandaa kuanza ajira yake mpya katika klabu ya Brighton.
Mei, mwaka huu, Ayto aliondoka Arsenal baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 10.
Aliondoka baada ya Arsenal kumuajiri Andrea Berta kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Michezo iliyokuwa wazi baada ya Edu kuondoka.
Kwa siku za hivi karibuni, mtaalamu huyo wa masuala ya usajili raia wa Italia amekuwa akihusishwa zaidi na Newcastle United.
Ikumbukwe, Ayto alikuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha usajili wa kiungo Martin Zubimendi aliyetua Emirates akitokea Real Sociedad.
Ikumbukwe, anaelekea Brighton baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa David Weir ataondoka hivi karibuni.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img