11.8 C
New York

Rais Samia aimaliza Morocco, aiwekea Stars mil. 200/-

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi Shilingi milioni 200 kwa wachezaji wa Taifa Stars endapo wataifunga Morocco.
Timu hizo zitavaana kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mtanange wa robo fainali ya michuano ya CHAN.
Aliyewasilisha ahadi hiyo ya Dkt Samia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi, alipoitembelea kambi ya Stars.
“Tuko hapa kwa niaba ya Rais Samia kufikisha pongezi zake kwa juhudi, nidhamu na kujitoa kwenu,” alisema Waziri Kabudi.
Mbali ya mchango wa Rais, pia Benki ya NMB imechangia kiasi cha Shilingi milioni 10, wakati Azam Media wametoa Shilingi milioni 50.
Tangu kuanza kwa michuano hiyo Agosti, mwaka huu, Stars imekusanya jumla ya Shilingi milioni 460, zikiwamo Shilingi milioni 20 kwa kila bao.
Wakati huo huo, Stars inafukuzia ubingwa wa michuano hiyo utakaoipatia Shilingi bilioni moja. Kufika fainali kutaipa Shilingi milioni 500. Hatua ya nusu fainali itaipa Shilingi milioni 200.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img