CATALUNYA, Hispania
BARCELONA wamempa mkataba mpya wa miaka miwili mlinda mlango wake raia wa Poland, Wojciech Szczesny.
Szczesny (35), alistaafu soka mwaka jana, kabla ya Barca kumsajili baada ya kipa namba moja, Marc-Andre ter Stegen, kupata majeraha.
Ter Stegen alipata majeraha hayo Septemba, mwaka jana, kisha akarejea dimbani wiki chache kuelekea msimu wa 2024-25.
Akiwa Camp Nou, Szczesny aliyewahi kuidakia Arsenal ametwaa mataji mawili; La Liga na Copa del Rey.
Kwa upande mwingine, hatua ya Barca kumpa mkataba mpya inaibua tetesi za Ter Stegen kuondoka klabuni hapo.
Ikumbukwe, Barca waliimarisha pia lango lao mwezi uliopita kwa kumsajili Joan Garcia kutoka Espanyol.
Arsenal ilimsajili Szczesny akiwa na umri wa miaka 16, kabla ya kuitumikia katika mechi 181.
Published:


