Na Mwandishi Wetu
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hillary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.
Marehemu Hillary ambaye amefanya kazi ya utangazaji katika vituo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikwamo BBC, inasemekana amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar, alifanya kazi Azam Media mwaka 2015 na 2023.
