Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dk. Lazaro Mambosasa amefungua mafunzo ya medani za kivita kwa kozi ya uafisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi namba 1.2024/2025 kwa lengo la kuwajengea uwezo hususani eneo la medani za kivita.

Akizungumza Mei 7, 2025 katika kambi ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga ambapo Dk. Mambosasa amewataka wanafunzi hao kuendelea kujifunza mbinu mbalimbali na kuzingatia weledi na maarifa wanayopatiwa ili kuongeza tija katika utendaji wao wa kazi za kila siku kwa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.
Aidha, Dk. Mambosasa amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa namna anavyoendelea kutoa fursa za kimasoma na mafunzo ya ndani na nje ya nchi kwa maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali ili kuwa na Jeshi la kisasa lenye viwango.