21 C
New York

Infographic| Tanzania tuko wapi chanjo ya Uviko-19

Published:

Tanzania imepokea dozi nyingine 800,000 za chanjo ya Uviko-19 aina ya Sinopharm kutoka Serikali ya China.

Waziri wa Afya, Ummy Malimu, amesema kuwa: “Tumepokea chanjo aina ya Sinopharm kwa ufadhili wa Serikali ya China jumla ya dozi 800,000 ambazo zitatumika kuchanja wananchi 400,000. Kwa niaba ya serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, naishukuru serikali ya China kwa kuwezesha upatikanaji wa chanjo hizi awamu ya pili kwa chanjo za aina hii awamu ya kwanza tulipokea jumla ya dozi 500,00 ambazo zilitumika kuchanja wananchi 250,000.

“Takwimu zaJanuari 25, 2022 jumla ya watu 1,922,019 sawa na 3.33% ya Watanzania walikuwa wamepata chanjo kamili. Tangu tuanze kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 hapa nchini hadi sasa tuna dozi 8,821,210 zikijumuisha Sinopharm, Janssen, Moderna na Pfizer ambazo zinatosha kuchanja jumla ya watanzania 5,082,380,” amesema Waziri Ummy.

Zaidi angalia usanifu wetu kupata uchambuzi zaidi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img