4.1 C
New York

Visual| Wizara ya Habari na Miaka 60 ya Uhuru

Published:

DESEMBA 9 kila mwaka, ni kumbukizi ya uhuru wa Tanzania kutoka kwa Waingereza na kwa mwaka huu itakuwa ni miaka 60 tangu ilipojitoa kwenye minyororo ya Wakoloni hao.

Kilele cha Siku ya Uhuru ni Alhamisi ya Desemba 9, 2021 ambapo hafla kuu inafanyika katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, kabla yakufikia kilele hicho cha miaka 60 ya Uhuru, Serikali kupitia Wizara zake mbalimbali imekuwa ikiainisha changamoto na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.

Miongoni mwa Wizara ambazo Mawaziri wamewasilisha mafanikio na changamoto katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru ni pamoja na ile ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Waziri mwenye dhamana hiyo, Dk. Ashantu Kijaji, ndiye aliyebanisha mafanikio mbalimbali, zikiwamo hatua muhimu zilizochukuliwa na awamu mbalimbali za Serikali katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafika hapa ilipo katika sekta ya habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Kwa mujibu wa Waziri Dk. Kijaji, mafanikio makubwa yameonekana ndani ya Tanzania kwa kuongezeka kwa vyombo vya habari, watumiaji wa huduma za simu pamoja na Intaneti.

Pia Minara ya mawasiliano imeongezeka hatua iliyoimarisha mawasiliano na uhakika wa mtandao katika sehemu kubwa ya Tanzania.

Mchanganuo

270- Idadi ya magazeti na machapisho yaliyosajiliwa.
200 – Idadi ya redio zilizosajiliwa.
48- Idadi ya vituo vya televisheni.
122 – Idadi ya blogu zilizosajiliwa
20- Idadi ya  redio mtandao zilizosajiliwa.
500- Idadi ya television mtandao (online TV) zilizosajiliwa.

1993- Mwaka ambao Serikali iliruhusu kuanzishwa kwa televisheni, redio na magazeti ya binafsi.
16,238 – Idadi ya simu za mezani zilizokuwapo wakati Tanganyika inapata uhuru.
71,405 – Idadi ya simu za mezani zilizoko sasa.

53,111,246 – Idadi ya laini za simu zilizopo sasa. 29,152,713 –Idadi ya watumiaji wa intaneti 29,152,713.

12,902 – Idadi ya minara ya mawasiliano, ambapo minara 2,630 inatoa huduma ya 2G na minara 9,579 inatoa 2G, 3G au/na 4G.

Bil 161 – Kiasi cha fedha kilichotumiwa na Serikali kuenga minara 1,068.
65% – Ya kata za Tanzania Bara zimetumika kujenga minara ya mawasiliano. Kwamba ujenzi umefanyika katika kata 2,579 kati ya 3,956.

92% – Ya kata 110 zimetumika katika ujenzi wa minara ya mawasiliano Zanzibar. Kwamba ni kata 101 ndizo zilizotumika kwenye ujenzi. 224 – Minara ya mawasiliano inayotarajiwa kujengwa, ambapo zabuni ya Sh bilioni 37.7 imeshatangazwa.

2010- Serikali ilianza kutekeleza Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi, mfumo unaotambulisha mahali halisi ambapo mtu anaishi, mahali ilipo biashara yake au ofisi anayofanyia kazi kwa kufuata jina la barabara na mtaa, namba ya nyumba au jengo pamoja na Postikodi.

Zaidi angalia(Visualization) usanifu wetu hapo juu…

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img