22.9 C
New York

Infographic| Uhaba wa ajira ulivyoguswa 2020/21

Published:

CHANGAMOTO ya uhaba wa ajira imekuwa kaa la moto duniani kote, hasa kwa nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzania, huku wahanga wakubwa wakiwa ni vijana.

Aidha, ongezeko la wasomi wanaohitimu elimu ya juu kila mwaka nayo imekuwa ikichagiza uhaba wa nafasi za ajira, hivyo dhana ya kujiajiri kuonekana kushika kasi.

Kama ambavyo imekuwa ikifanywa na mamlaka zingine duniani kote, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nayo haijachoka katika mapambano yake dhidi ya changamoto hiyo.

Ndiyo maana, imejaribu kuibua mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhaba wa ajira, ikiwamo kuajiri kupitia taasisi za umma.

Pia, Serikali imejaribu kwa kadri ya uwezo wake kuipa nguvu sekta binafsi, lengo likiwa ni kuifanya iweze kuajiri na kupunguza idadi kubwa ya wasio na ajira.

Kutokana na hayo, zimezalishwa ajira 450,416 hapa nchini kuanzia Julai 20 hadi Januari, mwsaka huu.

Katika idadi hiyo, 16,067 zilitoka moja kwa moja Serikalini, zikiwamo za ualimu (13,529), taasisi za Serikali (1,538) na udaktari (1,000).

Pia, Sekta binafsi ilizalisha ajira 280,941 kati ya hizo 450,416, huku miradi ya Serikali nayo ikiwapa ajira vijana 169,476.

Ajira hizo zilitengezwa wakati Serikali ikitekeleza Bajeti ya mwaka 2021-22, ambayo ni Tsh Trilioni 36.3, yaani ongezeko la asilimia nne ukilinganisha na Bajeti ya 2020-21.

Sehemu kubwa ya Bajeti hiyo (Sh trilioni 26) ilitokana na Fedha za Ndani, wakati Fedha za Nje,  kwa maana ya misaada na mikopo, ilichangia Sh trilioni 10.3 tu.

Wakati huo huo, Riba za Amana zilishuka kutoka asilimia 8.90 hadi 8.41. Ni kama ilivyokuwa kwenye Riba za Mikopo (16.28% hadi 15.72) na Mfumuko wa Bei (3.7% hadi 3.5) na hiyo ni kuanzia Januari hadi Desemba 2020.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img