MADRID, Hispania
USIKU wa kuamkia leo, kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham, alifunga bao moja na kutoa ‘asisti’ katika mchezo dhidi ya Elche.
Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2, matokeo ambayo yameirejesha Madrid kileleni mwa msimamo.
Zikiwa zimebaki dakika tatu mchezo kumalizika, wakati huo Madrid ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, Bellingham alitoa asisti kwa Kylian Mbappe aliyefunga na kuipatia Madrid sare hiyo.
Katika mchezo huo, Elche walipata pigo baada ya beki wake, Victor Chust, kulimwa kadi nyekundu zikiwa zimebaki dakika saba za mchezo baada ya kumchezea rafu Mbappe.
Matokeo hayo yameifanya Madrid kufikisha pointi 32, hivyo kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Barcelona inayoshika nafasi ya pili.
Kwa upande mwingine, kufunga na kutoa asisti ni mwendelezo wa kiwango bora cha Bellingham, ambapo amefikisha mabao matatu katika mechi nne za La La Liga alizocheza hivi karibuni.
Madrid watarejea dimbani Jumatano ya wiki hii kuikabili Olympiacos ya Ugiriki katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Published:


