14 C
New York

Amorim sasa amgeukia Anderson

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, amewataka mabosi wa klabu hiyo kufanikisha usajili wa kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson.
Awali, Man United walikuwa wakihusishwa zaidi na kiungo wa Brighton, Carlos Baleba, lakini Amorim ameonekana kubadili uelekeo.
Man United ilijaribu kumsajili Baleba wakati wa usajili uliopita lakini Brighton waligoma kumwachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 21.
Sasa, Amorim anamtaka zaidi Anderson wa Forest baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kuonesha kiwango bora msimu huu.
Hata hivyo, mabosi wa klabu ya Man United watalazimika kuweka mezani kitita cha Pauni milioni 100 ili kuinasa saini yake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img