14 C
New York

Beki Arsenal aumia akiwa kikosini Brazil

Published:

RIO, Brazil
KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, amesema beki wake, Gabriel, atafanyiwa vipimo baada ya majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya Senegal.
Gabriel amekuwa mchezaji muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal, ambayo imeruhusu mabao pekee katika mechi 11 za msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Nyota huyo alipata majeraha ya paja na kisha kutolewa wakati Bazil ikiumana na Senegal katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa jana jijini London.
Kuumia kwa Gabriel ni habari mbaya kwa kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, ambaye anajiandaa kuikabili Tottenham katika ‘derby’ ya London itakayochezwa Novemba 23, mwaka huu.
Baada ya mtanange huo wa Ligi Kuu, Washika Bunduki watashuka dimbani kuikabili Bayern Munich, ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img