LONDON, Uingereza
IMERIPOTIWA kuwa kuna mazungumzo yanayoendelea vizuri kati ya kambi za mabondia Anthony Joshua na Jake Paul.
Taarifa zinasema wawili hao watarushiana makonde katika pambano la ngumi za uzito juu na litapigwa Desemba, mwaka huu, mjini Miami.
Awali, Paul alitarajiwa kuzipiga na Gervonta Davis lakini pambano hilo limeota mbawa baada ya Mmarekani mwenzake huyo kukwaa kashfa ya unyanyasaji wa kingono.
Kwa sasa, Paul na kambi yake wanapambana kufanikisha pambano lake na Joshua na inasemekana kuwa mazungumzo yako kwenye hatua nzuri.
Gazeti la mtandaoni la Daily Mail Sport limefichua kuwa pambano hilo litapigwa Desemba 9 au 12.
Kabla ya kuibuka kwa taarifa hizi, promota wa Joshua, Eddie Hearn, alisema Muingereza huyo anahitaji pambano kali. “Tutafanya uamuzi wiki ii juu ya pambano linalofuata kwa Anthony,” alisema.
Published:


