14 C
New York

Wachezaji Nigeria wagomea mazoezi wakidai posho

Published:

LAGOS, Nigeria
MAANDALIZI ya timu ya soka ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Gabon yameingia mdudu baada ya wachezaji kugomea mazoezi wakishinikiza kulipwa posho zao.
Tukio hilo limetokea wakiwa mjini Rabat, Morocco, ambako ndiko utakakochezwa mchezo huo wa play off wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa, bado wachezaji wanadai posho zao zilizotokana na ushiriki wao katika mechi za kimataifa zilizopita.
Licha ya Shirikisho la Soka la Nigeria (BFF) kutokutoa taarifa rasmi, inaelezwa kuwa zipo jitihada zinazofanyika kumaliza changamoto hiyo.
Kwa sasa, kikosi cha Super Eagles kina wachezaji 23 kambini, wakiwamo Victor Osimhen, Alex Iwobi, Wilfred Ndidi, William Troost-Ekong, Calvin Bassey, Samuel Chukwueze na Ademola Lookman.
Kwa upande mwingine, hivi karibuni NFF waliwasilisha malalamiko yao kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakieleza kutokuwa na imani na waamuzi wa mchezo wao dhidi ya Benin.
Kile kilichoelezwa katika barua ya malalamiko, NFF wanasema waamuzi hao wanatoka Afrika Kusini na Benin, mataifa ambayo walikuwa nayo kwenye hatua ya makundi ya kufuzu fainali hizo za Kombe la Dunia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img