14 C
New York

CAF: Maandamano ya Morocco hayazuii Afcon

Published:

CAIRO, Misri
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limesisitiza kuwa fainali za mwaka huu za AFCON zitafanyika Morocco, licha ya hali tete ya usalama nchini humo.
Maandamano ya vijana yameshika kasi huko Morocco, wakipinga fedha nyingi zinazotumiwa na Serikali katika maandalizi ya fainali hizo.
Hoja ya vijana ni kwamba fedha hizo zingeweza kuelekezwa katika kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta za afya na elimu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Rais wa CAF, Patrice Motsepe, hakuna mkakati wa sasa wala wa baadaye wa kuipokonya Morocco nafasi ya kuandaa fainali hizo.
“CAF itashirikiana na Serikali na watu wote wa Morocco kuhakikisha AFCON inafanyika kwa kiwango bora zaidi kuwahi kutokea,” amesema Motsepe.
Wiki iliyopita, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Rachid El Khalfi, alisema watu 409 wanashikiliwa kutokana na maandamano hayo.
Wakati huo huo, raia 20 na polisi 260 wameripotiwa kujeruhiwa tangu maandamano hayo yalipoanza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img