14 C
New York

Russell afungashiwa virago

Published:

EDINBURGH, Scotland
MABOSI wa klabu ya Rangers wamejadiliana na kukubaliana kumfuta kazi kocha wake, Russell Martin.
Russell amefungashiwa virago akiwa ameliongoza benchi la ufundi katika mechi 17 pekee tangu msimu huu wa Ligi Kuu ya Scotland ulipoanza.
Katika mechi saba za Ligi, Russell mwenye umri wa miaka 39 alishinda moja pekee na ameiacha Rangers ikiwa nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu.
Uamuzi wa kumfukuza umekuja baada ya Rangers kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Bairns iliyopanda daraja msimu uliopita.
Baada ya dakika 90 za mchezo, polisi walilazimika kuingilia kati baada ya mashabiki wa Rangers kulizingira basi wachezaji wakiliimba jina la kocha huyo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, uamuzi wa kumtimua Russell umepata baraka za Mwenyekiti wa Rangers, Andrew Cavenagh.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img