10.9 C
New York

Dimitar Pentev; ‘CV’ ya UEFA, uzoefu soka la Afrika

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
SIKU chache tu zilizopita, Dimitar Pentev alitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania akiwa na kikosi cha Gaborone United ya Botswana.
Timu hiyo iliifuata Simba kwa mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya msimu huu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikumbukwe, Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya kwanza ugenini nchini, kabla ya kulazimishwa sae ya bao 1-1 ilipoikaribisha Gaborone United jijini Dar es Salaam.
Sasa, safari hii, Pentev ametua katika benchi la ufundi la Simba kuchukua nafasi ya Fadlu Davis aliyetimkia Raja Casablanca ya Morocco.
Kwa wasiomfahamu, ni kocha raia wa Bulgaria mwenye umri wa miaka 49 na ana leseni ya juu ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA).
Kama ilivyo kwa makocha wengi, Pentev aliwahi kucheza soka na alikuwa bora uwanjani akiwa katika eneo la kiungo.
Alipita katika klabu kadhaa za kwao, zikiwamo Cherno More na Chernomorets Byala, kabla ya kustaafu akiwa na kikosi cha Shabla mwaka 2011.
Miaka minne baadaye, alirudi uwanjani akiwa kocha-mchezaji wa Spartak Varna, wakati huo umri wake ukiwa ni miaka 39. Alistaafu moja kwa moja mwaka 2016.
Kabla ya kuajiriwa na Gaborone, aliwahi kupita katika mabenchi ya ufundi ya klabu za Victoria United (Cameroon) na FC Johansen (Sierra Leone).
Kwa miaka yake mitano ya kufundisha soka barani Afrika, ana heshima ya kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu. Alifanya hivyo akiwa Cameroon na Botswana.
Pentev amejiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea Gaborone United, ambayo aliinoa kwa miezi nane tu tangu alipoajiriwa Januari 23, mwaka huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img