10.9 C
New York

Savinho asaini miaka miwili Man City

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KIUNGO wa pembeni wa Manchester City, Savinho, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili klabuni hapo.
Savinho (21), huu ni msimu wake wa pili tangu alipotua Etihad akitokea Troyes kwa Pauni milioni 30.8 mwaka jana.
Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amecheza mechi 54 chini ya kocha Pep Guardiola, akifunga mabao manne na kutoa ‘asisti’ 12.
“Nimefurahi mno na najivunia kuona nimesaini mkataba mpya wa kubaki City,” amesema Savinho.
Tottenham walijaribu bila mafanikio kuinasa saini ya mchezaji huyo wakati wa usajili wa dirisha kubwa majira haya ya kiangazi.
Mwezi uliopita, kocha wa Man City, Guardiola, alitabiri kuwa Savinho atakuja kuwa mchezaji bora klabuni hapo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Soka wa Man City, Hugo Viana, naye alimzungumzia akisema:
“Savinho bado ana umri mdogo lakini ameonesha kiwango kikubwa, kinachotoa picha kuwa atakuwa mchezaji bora hapo baadaye.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img