10.9 C
New York

Alisson nje ya uwanja kwa wiki sita

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza
LIVERPOOL itamkosa kwa wiki sita mlinda mlango wake raia wa Brazil, Alisson, baada ya majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya Galatasaray.
Ni kwa maana hiyo, Liverpool haitamtumia kipa huyo katika mechi ya Jumamosi hii dhidi ya Chelsea na badala yake Giorgi Mamardashvili atasimama langoni.
Katika mchezo wa ugenini wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray mwanzoni mwa wiki hii, Liverpool ilifungwa bao 1-0 mjini Istanbul.
Mbali ya mechi hiyo, pia Alisson ataikosa Manchester United, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 19, mwaka huu.
Kama hiyo haitoshi, Liverpool haitaweza kumtumia Novemba 4, siku watakayoivaa Real Madrid, pamoja na mchezo wa Ligi Kuu utakaofuata dhidi ya Manchester City.
Habari njema kwa kocha wa Liverpool, Arne Slot, ni kwamba straika wake na kinara wa mabao kikosini, Hugo Ekitike, atakuwa fiti kuivaa Chelsea.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img