19.4 C
New York

Kocha Yanga: Hatukuwa na bahati kwa Mbeya City

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
BAADA ya suluhu katika mchezo wao wa leo dhidi ya Mbeya City, kocha wa Yanga, Romain Folz, ameeleza kilichowanyima ushindi katika mchezo huo.
Yanga walikuwa ugenini katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, ukiwa ni mwendelezo wa mechi za msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
“Tulijiandaa vizuri lakini tumekosa bahati ya kufunga mabao. Presha ya ushindi ilikuwa kubwa, kiasi cha kuondoa umakini kwenye eneo la ushambuliaji,” amesema Folz.
Kwa upande mwingine, kocha huyo alisisitiza kuwa Mbeya City imewapa changamoto ya maeneo ya kuimarisha ili kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.
Ni kwa matokeo hayo sasa, Yanga inafikisha pointi nne katika mechi mbili za msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Kabla ya kuifuta Mbeya City, ‘Timu ya Wananchi’ ilipata ushindi mnono wa mabao 3-0 ilipokutana na Pamba Mji katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Related articles

Recent articles