14.7 C
New York

Gyokeres ameanza kurudisha ‘chenji’ Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza
STRAIKA mpya wa Arsenal, Viktor Gyokeres, amefunga mabao mawili dhidi ya Leeds United, ikiwa ni mechi yake ya pili tu ya mashindano tangu asajiliwe na Washika Bunduki hao wa London.
Gyokeres, raia wa Sweden aliyesajiliwa akitokea Sporting Lisbon, alipachika mabao hayo katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Leeds United.
Jurrien Timber alikuwa wa kwanza kuitanguliza Arsenal, kabla ya kuweka ‘asisti’ kwa Bukayo Saka aliyefunga la pili.
Gyokeres alipachika bao la tatu, kisha Timber akarudi tena kwenye nyavu za wageni wa mchezo huo, Leeds United.
Aidha, mchezaji aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Noni Madueke, Max Dowman, alipata penalti baada ya kuangushwa kwenye boksi na Anton Stach na ndipo Gyokeres alipopiga na kufunga bao jingine.
Dowman ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili wa Arsenal kucheza mechi ya Ligi Kuu (EPL) akiwa na umri mdogo (miaka 15 na siku 234), akitanguliwa na Ethan Nwaneri (miaka 15 na siku 181) aliyeandika historia hiyo mwaka 2022.
Kabla ya mchezo kuanza pale Emirates, Arsenal walimtambulisha mchezaji wao mpya, Eberechi Eze, ambaye ametua akitokea Crystal Palace.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img