15.5 C
New York

Safari za nje zamponza Rais Sri Lanka

Published:

COLOMBO, Sri Lanka
RAIS wa zamani wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe, amekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya rushwa, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.
Taarifa zinaeleza zaidi, kwamba sehemu kubwa ya ‘upigaji’ ilikuwa katika safari zake za nje akiwa rais.
Akiwa Ikulu, mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 76 alisafiri nje ya nchi mara 23, ikigharimu kiasi cha Dola milioni 2.
Moja ya safari zake ni ile ya mwaka 2023 nchini Uingereza, ambapo alihudhuria sherehe za Chuo Kikuu cha Wolverhampton.
Uchunguzi umebaini kuwa Wickremesinghe alitumia fedha za umma, licha ya kwamba hiyo haikuwa safari ya kikazi.
Kabla ya kuwa rais, Wickremesinghe mwenye umri wa miaka 76 aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa nyakati tofauti katika miaka ya 1990.
Wickremesinghe anaingia kwenye historia ya kuwa rais mstaafu wa kwanza kufunguliwa mashitaka nchini Sri Lanka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img