15.5 C
New York

Mahakama yaagiza Rais Colombia aachiwe

Published:

BOGOTA, Colombia
MAHAKAMA Kuu nchini Colombia imeagiza Rais wa zamani wa nchi hiyo, Alvaro Uribe, kuachiwa baada ya awali kuhukumiwa kifungo cha ndani cha miaka 12.
Uribe mwenye umri wa miaka 73, amekuwa raia mstaafu wa kwanza wa Colombia kushitakiwa kwa makosa ya uhalifu.
Mwanasiasa huyo anashutumiwa kwa kusimamia ukiukwaji wa haki za binadamu akiwa madarakani kuanzia mwaka 2002 hadi 2010.
Wakati wa utawala wake, kwa mujibu wa waendesha mashitaka, jeshi lilihusika katika mauaji ya maelfu ya vijana.
Hata hivyo, Uribe amesema mara kadhaa kuwa mashitaka hayo hayana uhalisia, bali ni matokeo ya ‘siasa chafu’ za utawala wa Rais wa sasa, Gustavo Petro.
Uamuzi wa Mahakama umetaka Uribe awe huru hadi Oktoba, mwaka huu, ndipo utoke uamuzi wa mwisho.
Kwa upande wake, amepokea kwa furaha uamuzi huo wa Mahakama akisema: “Namshukuru Mungu, nawashukuru raia wenzangu wa Colombia kwa kuonesha upendo wao kwangu.”
Uribe ni mshirika mkubwa wa Marekani na hata Katibu Mkuu wa Taifa hilo kubwa kiuchumi, Marco Rubio, ameyataja mashitaka dhidi mkongwe huyo kuwa ni uonevu wa kisiasa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img