14.7 C
New York

Trump sasa ana kwa ana na Zelenskyy

Published:

KYIV, Ukraine
RAIS wa Marekani, Donald Trump, sasa amepanga kukutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy.
Mkutano huo utakaofanyika mjini Washington, DC, unakuja zikiwa ni siku chache tu baada ya Rais Trump kukutana na Vladimir Putin wa Urusi.
Bado Rais Trump anaamini jitihaza zake za kukutana na viongozi hao zitafanikisha kumaliza vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.
Baada ya kuzungumza kwa simu na viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) na NATO, Rais Trump alisema Mkutano wake na Putin ulikwenda vizuri.
Kwa upande wake, Putin amesema Mkutano wake na Rais Trump umeleta matumaini mapya ya kuona vita hiyo inafikia ukomo.
“Mazungumzo yalikuwa ya wazi na kwa upande wangu, yamesogeza karibu uwezekano wa kupata suluhisho,” alisema Putin.
Wakati huo huo, Zelenskyy ameonesha kuvutiwa na mpango wa kukaa mezani na Putin ili kumaliza uhasama unaoendelea kati ya mataifa yao.
“Mara zote Ukraine imekuwa ikiweka wazi jitihada zake za kupata usalama,” aliandika Rais huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘X’.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img