LOS ANGELES, Marekani
MEYA wa New Orleans, LaToya Cantrell, amefunguliwa mashitaka akituhumiwa kwa makosa ya rushwa.
Wakati huo huo, mashitaka hayo yamemuhusisha pia mlinzi binafsi wa mwanasiasa huyo, Jeffrey Vappie.
Waendesha mashitaka wameeleza kuwa LaToya na Vappie walikuwa karibu hadi pale mlinzi huyo alipostaafu mwaka 2024.
Wanasema hata baada ya kustaafu, bado LaToya aliendelea kumtumia mlinzi huyo ‘kutafuna’ fedha za umma.
Taarifa zinaeleza zaidi kuwa wawili hao walijinufaisha kupitia nyumba zinazomilikiwa na mamlaka za New Orleans.
Pia, Cantrell anatajwa kutumia si fedha za Serikali si chini ya Dola 70,000 kwa safari zake binafsi na Vappie.
Published:


