BOGOTA, Colombia
MGOMBEA urais katika Uchaguzi Mkuu ujao nchini Colombia, Miguel Uribe, amefariki akiwa na umri wa miaka 39 ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu alipopigwa risasi.
Akiwa kwenye kampeni mjini Bogota, Uribe ambaye ni Seneta, alijeruhiwa kwa risasi tatu, mbili zikilenga kichwani na moja ikimpiga mguuni.
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 anashikiliwa akihusishwa na tukio hilo, ingawa bado chanzo cha kufanya hivyo hakijafahamika.
Tukio hilo linakumbusha historia ya miaka mingi ya matukio ya wanasiasa chini Colombia kuuawa kwa kupigwa risasi.
Ikumbukwe, mama mzazi wa Uribe, ambaye ni mwandishi wa Habari mkongwe, Diana Turbay, aliwahi kuuawa na kundi la uhalifu la Los Extraditables mwaka 1990.
Published:


