24.2 C
New York

Madagascar kuzuia rekodi mpya Taifa Stars?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo itashuka dimbani kumenyana na Madagascar, ukiwa ni mtanange wa fainali za Africa kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Ushindi katika mtanange huo utaipa Stars tiketi ya kuingia hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Sasa, kuelekea mechi hiyo, rekodi zinaonesha kuwa timu hizo zina uzoefu wa kukutana mara tatu.
Katika mechi hizo, Stars imeshinda moja, imefungwa moja na kupata sare moja.
Madagascar walifungua pazia la michuano hii kwa suluhu (0-0) dhidi ya Mauritania lakini wana rekodi ya kuvutia kwenye mechi za makundi.
Hawajawahi kufungwa katika hatua hii tangu walipoanza kushiriki CHAN. Stars kuvunja mwiko huo?
Dhidi ya Mauritania, Madagascar hawakuwa bora. Walimiki mpira kwa asilimia 37 tu kwa dakika zote 90 za mchezo.
Katika mchezo huo, walimudu kupiga pasi sahihi 269, wakati Mauritania wao walikuwa na 532.
Mbaya zaidi kwao, walipiga shuti moja pekee lililolenga lango la Mauritania.
Kwa upande wao, Stars wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na ‘mzuka’ baada ya kuzifunga Burkina Faso (2-1) na Mauritania (1-0).
Wakati huo huo, Stars imeonekana kuwa na safu nzuri ya ulinzi, ikiwa haijaruhusu bao.
Katika historia ya CHAN, Stars imepoteza mechi moja tu kati ya saba za misimu ya hivi karibuni. Madagascar kutibua rekodi hiyo?
Mbaya kwa Stars ni rekodi zinazoonesha kuwa haijawahi kushinda mechi ya tatu ya hatua ya makundi katika michuano ya CHAN.

Related articles

Recent articles