MOSCOW, Urusi
MWANAUME raia wa Urusi, Bryan Kohberger, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani, licha ya kugoma kuzungumza mahakamani wakati wa usikilizaji wa kesi ya mauaji inayomkabili.
Kohberger alikuwa akishitakiwa kwa kosa la kuwaua kwa kuwachoma na kitu chenye ncha kali wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Idaho.
Tukio hilo lilitokea mwaka 2022, ambapo aliwavamia ndani kwao mjini Moscow.
Kohberger, tofauti na ilivyo kwa washitakiwa kujitetea, alikataa kuzungumza na imekuwa bahati kwake kukwepa adhabu ya kifo.
Hata hivyo, wapelelezi wameieleza mahakama kuwa hawakufanikiwa kubaini chanzo cha mauaji hayo wala uhusiano wa Kohberger na wanafunzi hao.
Katika hatua nyingine, waliieleza mahakama kuwa mshitakiwa hakuwahi kuwa na historia ya matukio ya uhalifu.
Published:


