BUENOS AIRES, Argentina
ALIYEWAHI kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, aliwahi kumuona shetani mara tatu kwenye maisha yake hapa duniani.
Francis aliliongoza Kanisa hilo kwa miaka 12 hadi alipofariki mwaka 2025 na hayo yameelezwa kwenye Kitabu chake kilichochapishwa hivi karibuni.
Katika kitabu hicho cha ‘“’The Private Diary of Pope Francis’ kilichoandikwa kabla ya kifo chake, anaeleza kuwa hatosahau alivyowahi kumuona shetani na kusikia sauti yake ya ajabu.
Ndani ya kitabu hicho kilichoandikwa kuanzia mwaka 1992 hadi 2024, kiongozi huyo wa kiroho alieleza kuwa amewahi kumuona shetani mara tatu kwenye maisha yake.
Akisimulia katika kitabu hicho, amesema mara ya kwanza alikuwa kwenye gari, mara ya pili kwenye ibada, na mara ya tatu akiwa kwenye kikao na viongozi wenzake wa Vatican.
“Sitosahau sauti yake ilivyo na nguvu,” ameandika Francis, akisisitiza pia kwamba hatosahau sauti ya macho ya kuisha aliyokuwa nayo shetani.
Aidha, kupitia Kitabu hicho, Papa Francis anasimulia alivyowahi kulala na kuiona milango ya jehanamu, akidai kuwa tukio hilo ni la Juni, 2018. ”Niliona milango ya jehanamu, iliniogopesha sana,” amesema.


